Sunday, April 24, 2016

KIZIMBANI KWA KUHIFADHI WAHAMIAJI HARAMU


Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga.

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Simon Kagoli amefikishwa mahakamani kwa kosa la kuhifadhi wahamiaji haramu nyumbani kwake na kuwatumikisha mashambani.

Kagoli ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kageji, anakabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kuishi na watu ambao sio raia, kuwasaidia raia wa kigeni kutenda kosa na kuajiri na kuwatumikisha wageni shambani mwake. Kesi hiyo namba 114/2016 iko mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Kibondo, Robert Male.

Mwendesha Mashitaka wa Uhamiaji, Richard Mwangole alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo kwa makusudi huku akijua kuwa kuhifadhi wahamiaji haramu ni kosa kubwa. Anatuhumiwa kuwafanyisha kazi wahamiaji hao na kuwalipa ujira wa Sh 110,000 kila mmoja. Male alikana makosa na yuko nje kwa dhamana.

Alidhaminiwa na wadhamini wawili, kila mtu kwa dhamana ya Sh milioni moja.

Related Posts:

  • Afisa Uchaguzi Halmashauri Ya Serengeti Ahukumiwa Miaka Saba Jela. AFISA uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara Bw.  Julius Bujabhi Makwasa amehukumiwa kifungo cha Miaka 7 jela baada ya kupatikana na hatia ya Makosa 34 yakiwepo ya Rushwa. Mnamo mwaka 2013 Taasi… Read More
  • UBAKAJI WA KITHIRI INCHINI Matukio ya ubakaji hasa kwa watoto wadogo yamekuwa yakiongezeka kwa kiwango kikubwa, ongezeko hili limebainika kutokana na ufuatiliaji tulioufanya kupitia matukio yaliyoripotiwa katika vituo vya Polisi ambapo katika kipi… Read More
  • ZITTO KABWE: MAKUNDI YA KIFISADI YAKABILIWE Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amemtaka Rais John Magufuli kukabiliana na vikundi vya mafisadi vinavyoiba mabilioni ya fedha za umma kupitia mikataba mibovu waliyoingia badala ya kuishia kutumbua majipu.… Read More
  • PICHA ZA UCHI ZAMFUNGA SIWEMA WA NEY WA MITEGO Wiki iliyopita zilianza kusikika taarifa mbalimbali kuhusu kuhukumiwa kwa mpenzi wa zamani na mama mtoto wa msanii Nay wa Mitego aliyehukumiwa kwenda jela miaka miwili  jijini  Mwanza. Pamoja na taari… Read More
  • Deni la Taifa Lafikia Trilion 33. 5 Deni la Taifa limeongezeka kwa Sh7.05 trilioni, kutoka Sh26.49 trilioni Juni 30, 2014, hadi Sh33.54 trilioni sawa na ongezeko la asilimia 27. Kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), … Read More

0 comments:

Post a Comment